KILIMO CHA MAHARAGE YA NJANO.
Kilimo cha maharage ni rahisi na kinalipa sana kikifanyika kwa utaalamu. Gharama nafuu na competion ya soko ni almost zero. Huhitaji kusafiri, kinachofanyika ni kuwaita wateja waje shamba watuniashane misuli mbele yako bila dalali kisha ww ndo una decide whom to trade with!
Ekari moja ya maharage ya njano unaweza pata gunia 20 - 30. na gunia moja kwa sasa ni shs 270,000.
Shamba la maharage kama unalima kwa kumwagilia unaweza lima mara tatu kwa mwaka . Hii ina maana ukilima ekari moja tu utakua na uhakika wa kipato cha Milioni 5.5 kila baada ya miezi minne, na kama ukilima ekari kumi basi wewe kila miezi minne utakua unaingiza milioni 55. Hata uwe mlevi vipi huwezi maliza hizo helaa na ni lazima baada ya mwaka mmoja tu mabenki yataanza kukuheshimu na status yako itabadilika for good. Sasa baada ya kukupagawisha na kukuchanganya juu ya mill 55 kila baada ye miezi minne ndugu mdau wa CHAKULACOM na mkulima mwenzangu sasa twende tukalichambue harage la limwa vipi
Maharage ni lishe ya pili kwa umuhimu nchini Tanzania baada ya mahindi. Maharage yanaweza kuliwa yakiwa
machanga/mateke (green/French beans) na yakiwa mabichi au yamekauka baada ya kukomaa.
Maharage ni chanzo muhimu cha protini kwa binadamu na husaidia udongo katika utengenezaji wa madini ya nitrogen
kutoka kwenye hewa kwa kupitia mizizi ya maharage ambayo husaidiana pamoja na rhizobium/ryzobium bacteria
kwenye udongo. Nitrogen ni muhimu kwa ukuaji na uzalishaji wa mahindi.
Kwa miaka mingi maharage yamekuwa yakilimwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani lakini hali inabadilika kwasababu
soko la maharage limekua, bei yake kuongezeka na mahitaji ya maharage yameongezeka. Hii imesababisha kuongezeka
kwa uzalishaji na biashara ya maharage nchini na nje ya nchi.
Matumizi ya Maharage
Maharage hutumika kama chakula cha binadamu na pia majani yake huweza kutumika kama chakula cha mifugo. Katika
chakula cha binadamu maharage hutumika kama kiambatanishi (mboga) cha vyakula vingine kama vile wali au ugali.
Faida za maharage
a) Mbegu
Mbegu za maharage zina viwango vingi vya protini ambavyo ni muhimu katika kujenga mwili kwa sbababu yanatoa
proein; hivyo hutumika badala ya nyama, madini ya magnesium husaidia katika afya na ukingaji wa moyo kutoka kwenye
maradhi, madini chuma husaidia kuupa mwili nguvu, Vitamin B1 (Thiamin) na Vitamin K huongeza uwezo wa
kumbukumbu hivyo kuwa muhimu kwa watu wenye matatizo ya kupoteza kumbukumbu.
Maharage ni chanzo kizuri cha kupunguza cholesterol mwilini, cholesterol nyingi mwilini ni chanzo cha magonjwa
mengi. Pia maharage husaidia kukinga viwango vya sukari kwenye damu kuongezeka ghafla baada ya mlo, hivyo ni
muhimu sana kwa watu wenye kisukari. Zaidi ya yote vyakula vya jamii ya maharage vimeonekana kupunguza
uwezekano wa kupata mshituko wa moyo. Tafiti za hivi karibuni zimegundua kuwa ulaji wa maharage hupunguza
uwezekano wa kupata saratani (cancer) tofauti na nyama ambayo huongeza uwezekano wa kapata saratani.
i) Majani na maua ii) Maharage iii) Maharage machanga
b) Majani
Majani ya maharage pia huweza kutumika kama mboga na katika baadhi ya jamii za watu nchini, majani mateke ya
maharage huchumwa na kukatwakatwa kisha kupikwa kama mchicha au mboga nyingine yoyote ya majani.
Upandaji wa Maharage
1.Mbegu
Upandaji wa maharage unatakiwa ufanyike katika muda muafaka kutokana na eneo ili kuweza kupata maji ya kutosha
(mvua) na wakati wa mavuno kunatakiwa kuwe na ukavu ili maharage yasiharibikie shambani. Maji mengi yaliyotuama
na ukame siyo nzuri kwa maharage na husababishia mmea magonjwa na kuoza au kukauka� Kuna aina nyingi za maharage ambazo zinaweza kupandwa kwa mfano (Rojo, Mshindi, Pesa, SUA 90 na Canadian
wonder) ambazo ni mbegu zilizoboreshwa, lakini pia kuna mbegu za kawaida zilizopo kwa wakulima ambazo huhimili
baadhi ya magonjwa na wadudu.
Inashauriwa kupanda maharage katika umbali wa (50×20) sentimita 50 (mstari kwa mstari) na sentimita 20 (mmea kwa
mmea), panda mbegu mbili za maharage katika shimo moja, mbegu zinaweza kupandwa katika umbali wa sentimita 3-6
kwenda chini. Kama mbegu moja moja katika kila shimo, nafasi itapungua. Kwa maharage yaliyokuwa vizuri kunatakiwa
kuwe na idadi ya mimea 150,000-200,000 kwa hekta (maharage mafupi), maharage yatambaayo idadi yake ni nusu ya
maharage mafupi kwa hecta. Hekta 1 = ekari 2.471.
2.Mbolea
Mimea huhitaji virutubisho kutoka kwenye udongo ili kuweza kukua na kuzalisha matunda yenye afya. Maharage huhitaji
madini ya phosphorous na potassium ambayo hupatikana kutoka kwenye mbolea hai kama vile samadi, mboji, majivu,
mkojo wa mifugo na mabaki ya mimea. Ni muhimu kufahamu udongo ambao unatarajia kupanda mimea yako ili
kutathmini viwango vya madini yaliyopungua ili kufanya juhudi za kuongeza.
Zaidi ya yote ni vizuri kutumia mbolea hai ambazo zinasaidia viumbe hai huweza kukua na kuendeleza kurutubisha
udongo, kwa mfano mizizi ya maharage husaidiana na viumbe hai (nitrogen fixing bacteria) waishio kwenye udongo
kutengeneza nitrogen. Mbolea za chumvichumvi huharibu na kufukuza viumbe hai kutoka kwenye udongo.
3.Magugu
Inashauriwa kupalilia mimea kabla haijatoa maua. Shughuli hii inatakiwa ifanywe kwa uangalifu ili kukinga mimea
isiharibike kwenye mizizi kwani uharibifu wa aina yoyote huweza kusababisha magonjwa kwa mmea. Inashauriwa
kupanda mimea kwa kuzunguka (crop rotation) ili kupunguza uwezekano wa magugu na mardhi kuweza kushambulia
mimea.
4.Wadudu na magonjwa
Maharage hushambuliwa na wadudu na magonjwa. Miongoni mwa njia
za kuzuia, kukinga na kufukuza wadudu ni kuhakikisha kuwa mimea
ipo katika hali nzuri (imepaliliwa, nafasi ya kutosha na haijaharibika).
Pia kubadilisha aina ya mimea inayopandwa kwenye shamba moja mara
kwa mara husaidia kupunguza uwezekano wa wadudu kuongezeka.
Kwa baadhi ya wadudu kama vile viwavi (African Ballworm) huweza
kufukuzwa kwa kutumia muarobaini au vitunguu saumu. Maji ya
muarobaini ni dawa nzuri sana kwaajili ya kufukuzia wadudu na haina
madhara yoyote kwa binadamu.
5.Kukomaa na Kuvuna
Maharage ya kijani yanatakiwa yavunwe kabla punje za maharage hazijakuwa sana. Hii ni kati ya wiki 7-8 baada ya
kupanda. Maharage makavu huvunwa mara tu kiasi cha kuridhisha cha kukomaa na kukauka kinapokuwa kimefikiwa.
Kwa mfano asilimia 80 ya maharage yakishakomaa na kuanza kubadilika rangi (kukauka) au kwa aina nyingine kusinyaa
yanakuwa tayari kwa mavuno.
Kwa kawaida mmea wote hung’olewa na kuwekwa juani ili uendelee kukauka kisha maharage hutolewa kutoka kwenye
mmea na kuendelea kukaushwa ili kupunguza matatizo wakati wa kuhifadhi. Baada ya kukauka hadi kufikia angalaua
asilimia 12 ya unyevu, maharage yanatakiwa yahifadhiwe kwenye chombo chenye mfuniko kama vile ndoo ya plastiki au
pipa na kuendelea kuyaangalia mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa wadudu hawajaingia na kisha kuyafunika tena.
6.Kilimo mchanganyiko
Ni vizuri sana na inashauriwa kupanda maharage pamoja na mimea ya jamii nyingine kama vile mahindi kwani husaidia
katika kusambaza madini ya nitrogen na kwa maharage yenye kutambaa, hupata sehemu ya kujishikilia au kutambalia.
Maharage yanaweza yakapandwa katikati ya mistari ya mahindi. Pia viazi huweza kupandwa pamoja na maharage.
Inashauriwa kutokupanda maharage pamoja na mimea mingine ya jamii ya maharage (leguminous) kwani husababisha
mimea isiweze kukua vizuri kwasababu ya kutokupata virutubisho vya kutosha na huweza kusababisha matatizo kama �ya wadudu kama nzi weupe.
Mbegu za maharage ya njano F1 za Muda wa siku 85 zinazohimili ukame
No comments:
Post a Comment