Jinsi ya kutengeneza chakula cha nguruwe
Wakati wa kutengeneza chakula cha nguruwe inabidi kuzingatia yafuatayo:
• Mchanganyiko wake uwe na viinilishe vinne vilivyotajwa hapo juu
• Chagua aina ya viinilishe vinavyoweza kupatikana kwa urahisi na bei nafuu kwenye mazingira yako
• Aina ya mchanganyiko wa chakula ni muhimu uzingatie mahitaji ya nguruwe kama umri (mfano: nguruwe wanaonyonya, waliochishwa kunyonya, wanaokua, na wanaonyonyesha)
Mifano mbalimbali ya vyakula vya nguruwe.
1. Mchanganyiko namba 1: inapendekezwa kwa wafugaji walioko kwenye mazingira ambayo pumba za mahindi na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi
2. Mchanganyiko namba 2: kwa wale ambao pumba za mahindi, za mpunga machicha ya pombe na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi.
3. Mchanganyiko namba 3: kwa wale ambao pumba za mpunga na mahindi yanapatikana kwa urahisi.
. Kiasi na namna ya kulisha
• Nguruwe wanahitajika kulishwa aina hii ya chakula mara mbili (asubuhi na mchana) au zaidi kwa siku
• Kiwango/kiasi cha kulisha kwa nguruwe wa aina na rika tofauti .
• Pamoja na vyakula vilivyotajwa, wafugaji wanashauriwa kuwapatia nguruwe vyakula vyao vya kijadi karna vyakula vya ziada mfano, majani mabichi laini HYDROPONIC, majani ya maboga, mbogamboga, matunda kama maparachichi, majani ya viazi n.k.
Viwango vya kulisha nguruwe wa uzito mbalimbali
Na Wakati Uzito wa nguruwe (kilo) Kiasi cha chakula (kilo kwa siku)
1. Baada ya kuachishwa 10-17 0.75
kunyonya hadi uzito kiasi
2. Uzito uliozidi kiasi kidogo 18 - 29 1.00
3. Uzito wa kawaida 30- 40 1.50
4. Uzito mkubwa kiasi 41 - 60 2.00
5. Uzito mkubwa 61 - 80 2.5
6. Uzito mkubwa sana 81 - 100 3.00
7. Nguruwe anaye nyonyesha 120 - 150 6.00
Jinsi ya kulisha jike la nguruwe kabla na baada ya kuzaa
Kipindi cha mimba, kuzaa hadi kuachisha kunyoyesha
Kipindi cha miezi mitatu baada ya kupandishwa
•Apatiwe chakula kiasi karna kilo mbili kwa siku
•Kiasi hiki kiendelee hadi wiki 3 kabla ya kuzaa
Wiki tatu kabla ya kuzaa
•Ongeza chakula kufikia kilo mbili na nusu.
1.3 Wiki moja kabla ya kuzaa
• Anza kuopunguza chakula taratibu hasa vyakula vya nafaka (Concentrate rations).
• Ongeza vyakula vya mbogamboga, majani laini na matunda (laxative meals).
Siku ya kuzaa
• Usimpe chakula chochote cha nafaka.
• Mpe vyakula vya mbogamboga,na vilaini kwa kiasi kidogo tu
• Mpatie maji ya kutosha.
Siku ya 1 - 2 baada ya kuzaa
• Mpe nusu kilo ya chakula kamilifu.
Siku ya 3 na kuendelea
• Ongeza chakula cha nafaka kwa kiasi cha kilo 1 kwa siku.
• Ongeza kufikia kiwango kinachohitajika kulingana na idadi ya watoto alionao mama nguruwe.
Zingatia
• Mama nguruwe anahitaji kilo 3 za chakula kwa matumizi yake ya kawaida.
• Atahitaji kiasi cha ziada cha theluthi moja (1/3) ya kilo ya chakula kwa kila mtoto aliyenae
Mfano: kama mama ana watoto 9 atahitaii kiasi ani cha chakula?
Mahitaji mama peke yake Mahitaji kutokana na watoto Kiasi cha chakula kwa siku
3kg Theluthi moja x 9: (113 X 9 =
3 Kg) 3 kg + 3 kg = Kilo 6 kwa siku
Endelea kumpa kiwango hicho cha chakula mpaka ifikapo wik:i moja kabla ya kuwaachisha watoto kunyonya.
Wiki moja kabla ya kuwachisha punguza kiwango taratibu mpaka kufikia kilo 3 kwa siku
Baada ya kuachisha kunyonya
• Mama nguruwe wapatiwe chakula bora kilicho na kiwango kikubwa cha maclini na vitamini kiwango cha kilo 2 - 3 kwa siku.
• Hii itamsaidia kuivisha mayai, hivyo kumsaidia kupata joto mapema.
No comments:
Post a Comment