Friday, 5 October 2018

UPISHI WA DONATS

Donats

Unga Wa Ngano Vikombe ( 3 )

Sukari Vijiko ( 3 )

Maziwa Vijiko ( 3 )

Mayai ( 3 )

Siagi Ilioyeyushwa Vijiko ( 3 )

B.P Kijiko Kidogo ( 1 )

Hiliki/Vanilla Ukipenda

Mafuta Ya Kupikia

Unachanganya Sukari / Mayai Kwa Mchapo Wa Keki / Mashine Ikichanganyika Na Sukari Unaweka Maziwa / Siagi Unachanganya Tena Iwe Mchanganyiko Mmoja Kisha Unachanganya Unga Na B.P Kisha Unakanda Unga Kwa Kutumia Yale Mayai Uliochanganya Na Maziwa Ukisha Kuwa Donge Weka Kwa Muda Wa Dakika 10 Kisha Anza Kusukuma Kama Chapati Kisha Unakata Kwa Kutumia Kikombe/Glass/Kikopo Utakata Mara Mbili Kwanza Duara Kubwa Kisha Utakata Duara Dogo Weka Mafuta Yakipata Moto Unaanza Kupika Kama Maandazi Ukimaliza Wacha Zipowe Kisha Saga Sukari Uzinyunyizie
Tayari Kwa Kahawa/Atai
Enjoy

Cheif 🍧 Yum 🍮 Yum 🍩

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO