Monday, 15 October 2018

JINSI YAKUTENGENEZA SABUNI YA KUNAWIA MIKONO NA YA KUSAFISHIA VYOO

Sabuni ya maji   sabuni ya kunawia mikono.   Kusafishia vyoo

Malighafi kuu ni

1*Sulphonic acid (salfoniki asidi)

2*silesi au ungaroli

3*chumvi

4*manukato

5*rangi ya sabuni

Malighafi za kawaida (hazina ulazima)

1*soda ash

2*griselin

3*formalin nk

Katika malighafi zote malighafi mama ni salfoniki na siles

Pia unaweza kutoa Sabin kwa kutumia sulphonic acid bila siles

Pia unaweza kutoa sabuni kwa kutumia siles bila sulphonic acid

👇🏽
Utengenezaji Wa sabuni

  Andaa ndoo ya Lita 20 weka maji Lita 10

Baada ya hapo anza kukoroga maji kuelekea upande mmoja

Kisha unakoroga mwengne aanze kumimina sulphonic acid nusu Lita

Baada ya hapo mimina siles nusu Lita

Baada ya hapo mimina rangi kiasi upendacho ww

Baada ya hapo mimina manukato kiasi upendacho ww

Kama ukiwa na haya material

Mimina soda ash vijiko viwili vya chakula

Kisha mimina griselin robo Lita

Kisha weka formalin vijiko 5 vya chakula

Kumbuka usiache kukoroga

Baada ya hapo weka chumvi viganja wivili vya mkono

Baada ya kumaliza kuchanganya malighafi zote endelea kukoroga kwa dakika 15

Baada ya dakika 15 sabuni itakua tayari

Nb malighafi za kwanza kuanza Nazi ni sulphonic au unagalor alafu zingne utakazo penda wewe ila chumvi iwe ya mwisho

1 comment:

  1. Kutengeneza hii sabuni kwa ujazo wa lita 5 wengine wanasema tutumie symphonic acid viboko vitano vya chakula. Wewe kutengeneza ya ujazo wa lita 10 unasema tutumie sulphonic acid nusu lita. Mnatuchanganya mno hii sabuni ni ya kunawa mjue sasa vipimo vinanipa mashaka sijui nani mkweli maana hapa ukikosea kidogo utachubua na kuunguza watu mikono yao.

    ReplyDelete

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO