BIASHARA GANI NI ZURI AMBAYO INALIPA NAWEZA KUIFANYA KWA SASA?
Kwa ufupi ni kwamba Biashara nzuri ni ile unayoipenda na unayoiweza kuifanya vizuri na kwa ubora tofauti na wengine lakini ni lazima uwe na muda Wa kuisimamia,vinginevyo itafeli.
Biashara nzuri zaidi ni Biashara inayohusika na kutatua matatizo ya watu katika eneo lako unapoishi au unapofanyia kazi. That's all about Business.
Ukitaka kufanikiwa ktk Biashara ni lazima
1.Uipende Biashara yako.
2. Uwe na muda Wa kuisimamia.
3. Uwe na uwezo Wa kuifanya na uifanye kwa uzuri na ubora Wa hali ya juu tofauti na washindani wako.
4.Uwe na Elimu au maarifa sahihi kuhusu Biashara unayotaka kuifanya.
5.Uwe na washauri wazuri ktk Biashara yako yaani Uwe na watu walioifanya na wanaoifanya Biashara hiyo na ambayo wamefanikiwa ktk hiyo biashara. Ni hatari kubwa kuwa na washauri ambao eidha walifeli ktk hiyo Biashara au wasiofanya hiyo Biashara wengi wao watakukatisha tamaa na kukuvunja moyo.
Huu ni mfano hai ambao Mimi Binafsi nauamimi na nimenufaika nao sana. Nilipotaka kuoa niliwauliza watu ambao wameoa na wanaishi vizuri ktk ndoa zao,nilipotaka kusoma fani ya uinjinia niliwauliza watu waliosoma na kunufaika na Elimu hiyo, nilipotaka kujenga niliwauliza watu waliojenga na nilipotaka kufungua Biashara niliwauliza watu sahihi wanaofanya Biashara hiyo na kamwe sijawahi kujuta ktk maamuzi Yangu namshukuru Mungu kwa hilo.
Angalizo Akili ya kuambiwa changanya na yako. Sio kila ushauri utakufaa ila ni muhimu kutafuta ushauri then baada ya ushauri ukae chini mwenyewe utafakari na ujiridhishe kama ni sahihi ufanye na kama sio sahihi tafuta njia nyingine.
Utajuaje kama ushauri uliopewa na mentor wako kuwa ni sahihi ama sio sahihi?
Akili ya kuzaliwa na kujifunza inakuhusu. Huwezi kufanikiwa ktk jambo lolote kama huna maarifa au Elimu nacho. Tafuta maarifa na Elimu,jifunze ili uelewe vizuri juu ya kitu unataka kufanya kabla ya kufanya maamuzi yako. Hapa ndipo watu wengi hukosea na kutuja baadae. Huwachukia waliowashauri kwa kuwasababishia matatizo ktk Ndoa zao,Biashara zao na hata maisha yao kwa ujumla kwa sababu walichukua ushauri na kufanya walivyoambiwa bila kuchunguza au kutafakari kwanza.
Usikurupuke ktk maisha utajuta na kujilaumu au kuwalaumu wengine bure usipojiongeza.
Katika Maisha ya mafanikio hakuna njia ya mkato. Ukitaka shortcut lazima ujiandae kusubiri maumivu ya majuto baadae. Kutafuta shortcut ktk maisha ni kuogopa kulipa gharama Leo na kusubiri kuja kulipa baadae.
So ukitaka kufanikiwa ni lazima ufuate Sheria,kanuni na miiko ya Mafanikio otherwise usitafute Wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu mwenyewe.
No comments:
Post a Comment