Monday, 8 October 2018

UFUGAJI WA MBUZI AINA YA BOER

MBUZI BOER

  

Kiasili ni mbuzi wa Afrika ya kusini ingawa ndani yake kuna damu toka baraUlaya na India, hii ndio Mbegu kubwa Zaidi ya mbuzi wa nyama ukilinganisha na wengine. Pia wanazalisha kiwango kikubwa cha maziwa ingawa wanafaa Zaidi kwa nyama.

RANGI
Wana mwili wenye rangi nyeupe na kichwani wana rangi nyekundu au hudhurungi (brown) ingawa wapo weupe kabisa au wekundu/hudhurungi kabisa na hii hutokea kwa 0.001%

UMBO
Wana umbo kubwa kufikia kilo 110-135kwa madume
Kilo 90-100 kwa majike
Wana masikio yaliyolala kama mbuzi wa kinubi (Nubians)

UZAZI

Huwa wanazaa mapacha na huweza kuzaa mara 2 kwa mwaka
Majike ni wazazi na walezi wazuri wa watoto sababu wana maziwa ya kutosha
Watoto hukua haraka sana, na nia aina ya mbuzi ambao sio wakorofi (docile)
Kwenye baridi kali au joto kali huwa inawaathiri kwenye kubeba mimba
Ufugaji wa mbuzi ni utajiri uliyojificha. Kwanza huzaliana kwa haraka kwa maana kwamba kwa mwaka mmoja mbuzi mmoja ana uwezo wa kuzaa mara mbili lakini vilevile hawasumbui kwenye masoko. Wanakula majani zaidi kwa kuwa wao ni aina ya wanyama wenye matumbo manne yaani Ruminant animals ambao kwa kiasi kikubwa hutegemea zaidi  majani kama chakula chao kikuu. Mbuzi si kama kuku ambao huhitaji chakula  kilichotengenezwa maalum na kwamba kila siku watahitaji utoe pesa yako mfukoni  kwa ajili ya kuwanunulia chakula. Mbuzi wanauwezo wa kuishi wenyewe bila kuhitaji hela yako ya mfukoni kwa ajili ya chakula kwa muda mrefu ilimradi tu wawe wazima. Ni muhimu ukawa na daktari wako maalum ukaingia nae mkataba kusudi kila baada ya muda fulani awe anakufanyia ufuatiliaji wa maendeleo ya mbuzi wako japo kwa mwezi mara moja na pale linapotoke tatizo hasa mripuko wa ugonjwa. Kutokuwa na daktari wa mifugo katika mradi wako wa ufugaji wa mbuzi ni sawa na kutembea barabarani huku ukiwa umefungwa kitambaa usoni.  Daktari wa mifugo si lazima umtoe mbali, kila kijiji kuna madaktari hao au maafisa mifugo ambao unaweza ukaongea nao mmoja wapo ili awe anakupa huduma pale inapohitajika ila kama utakwama kabisa sisi CHAKULACOM tunamadaktari wenye weledi mkubwa kuhusu mifugo tuite tutakuhudumia .

Mbuzi wanahitaji uwe na shamba kubwa lenye maji ya kutosha na majani. Pia kuwe na vijana wa kazi waaminifu kwa ajili kuwachunga na ulinzi. Na ni muhimu pia shambani kukawa na Mbwa kwa ajili ya kuongeza ulinzi katika mradi wako.

Tanzania tuna mapori makubwa ambayo unaweza ukafanya uendeshaji wa mradi wako wa ufugaji wa mbuzi kwa ufanisi mkubwa bila kujali ni umbali kiasi gani. Watakapokuwa tayari kuvunwa, utatafuta gari na kuwapakia mbuzi wako na kisha kuwapeleka mnadani ambako utawauza kirahisi sana. Kuna minada mingi ya mifugo hapa Tanzania. Kuna ile minada ya awali ambayo wafanyabiashara wa mifugo wanaenda kuchuuza huko na kuwapeleka kwenye minada ya upili ambayo ni minada mikubwa iliyo chini ya wizara ya mifugo. Sasa kwa mfugaji wa mbuzi, utaamua wewe mewe mwenyewe kama uwapeleke mnada wa awali au mnada wa upili. Lakini vilevile kwa sasa kuna  machinjio za kisasa za mifugo mfano machinjio ya kisasa ya mifugo ya  Kizota Dodoma mjini ambayo mahitaji mbuzi yamekuwa makubwa kupita maelezo kutokana na nyama yake kuhitajiwa zaidi katika nchi za kiarabu hasa Oman na Dubai. Kwahiyo mahitaji hayo ya mbuzi yametengeneza soko kubwa na la uhakika. Shughuli za kilimo katika ufugaji hazisumbuliwi sana na masoko kama zilivyo shughuli za kilimo cha mazao mfano nafaka na matunda kutokana na kwamba minada minada ya mifugo imekuwa mkombozi mkubwa kwa wafugaji.

Changamoto katika ufugaji wa mbuzi ni magonjwa ambayo kimsingi yanadhibitika kupitia wataalamu wa mifugo.

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO